Windows

Adungwa kisu kwa kufumaniwa na mke wa mtu kitandani



Maisha ya kibarua mmoja (house boy) katika Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya yako hatarini baada ya kudungwa kwa kisu na mwanamume ambaye alimpata kitandani na mkewe.

Inadaiwa kuwa mume huyo alikuwa ameondoka nyumbani kuelekea kazini Jumatatu asubuhi, lakini akagundua alikuwa amesahau kitambulisho.

Hata hivyo, aliporejea nyumbani alishangaa kumpata mfanyakazi huyo kitandani na mkewe, ndipo akapandwa na hasira na kuchukua kisu, akamdunga mikononi na sehemu nyingine za mwili, akimsababishia majeraha tele mwilini.

Mshukiwa alipiga mayowe akitafuta usaidizi, nduru zake zikiwavutia wakazi wengi ambao walimwokoa na kumkimbiza katika hospitali ya kibinafsi ya White Rose, ambapo bado anatibiwa baada ya kushonwa majeraha.

Mume husika alikamatwa na polisi wa utawala eneo hilo na bado anazuiliwa akihojiwa, wakazi wakisema alikuwa karibu kumuua mfanyakazi huyo.



Post a Comment

0 Comments