Bondia raia wa Urusi Maxim Dadashev ameaga dunia baada ya pambano lake na Subriel Matias kumsababishia majeraha makubwa ya ubongo siku ya Ijumaa.
Dadashev, 28, alishindwa kutembea baada ya pambano hilo ambalo mkufunzi wake Buddy McGirt alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali bila majibu.
Dadashev alikimbizwa hospitali ambapo madaktari waligundua damu ilikuwa ikimvuja kwenye ubongo.
0 Comments