

Shindano la vijana kuhusu biashara linaloungwa mkono na Benki ya Dunia kwa lengo la kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira limezinduliwa nchini Kenya.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Eritrea, Kenya, Rwanda na Uganda Bw. Carlos Felipe Jaramilo, amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa benki hiyo imetenga dola milioni 13.5 kwa ajili ya shindano la mpango wa biashara la Mbelena, ambalo litatoa mtaji kwa watu 750.
Amesema shindano hilo litakalofanyika katika nchi nzima, litawalenga vijana wenye mawazo ya kufanya biashara, au ambao tayari wana biashara, na lengo lake ni kutengeneza nafasi za ajira kwa vijana.
Amesema shindano hilo litawalenga zaidi wanawake ambao huwa hawashiriki sana kwenye mashindano kama hayo.



0 Comments