

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo waache kuingilia majukumu ya kiufundi yanayofanywa na benchi la ufundi na viongozi wakati huu wa usajili
Manara amewakosoa wale wanaoponda usajili wa beki Kennedy Juma aliyesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
"Kuna wakati mashabiki wetu mnakosea na ndio maana vitu vingine hatuvijibu, yaani mko kwa ajili ya kulaumu laumu wakati wote kuliko kuja kushauri," amesema Manara
"Huyu mchezaji mmayehoji ubora wake ni kocha ndiye aliyetaka mlinzi wa kati mwingine"
"Hatuwezi kusajili wachezaji wote wa kigeni kwa kuwa nafasi zilizopo ni kumi ambazo pia tayari Waziri ametaka zipunguzwe wabaki watano"
"Sasa tusajili wachezaji wote wa kigeni? ina maana hatupaswi kusajili wachezaji wazawa kabisa?"
"Kila mchezaji mzawa anayesajiliwa Simba lazima mashabiki wetu mkatae mwanzoni"
"Ilikuwa hivyo kwa Bocco ambaye alipachikwa majina mengi sana lakini ndiye anayetubeba akishirikiana na wachezaji wengine"
"Bocco amefunga mabao zaidi ya 40 tangu alipojiunga na Simba miaka miwili iliyopita"
"Ni vyema tukaacha taaluma zikafanya kazi yake, kama kocha amemuona mchezaji na kutaka asajiliwe hatupaswi kupinga kwani sisi mashabiki hatuna utaalam zaidi yake"



0 Comments