

Aidha Harambee ya kuichangia timu hiyo iliyofikia kilele juzi ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ilifana sana na kuipa Yanga uhakika wa kuanza msimu mpya ikiwa vizuri kiuchumi
Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji wasiopungua 11, nane tayari wametambulishwa huku wengine wakisubiri michakato yao ikamilike waweze kuwekwa hadharani
Hali ni tofauti kwa wapinzani wao Simba, ambao mpaka sasa hawajaweka hadharani jina la mchezaji mpya kutoka nje ya nchi licha ya tambo nyingi za kuwa na uwezo wa kusajili mchezaji yeyote Afrika
Mpaka sasa Simba imewaongezea mikataba wachezaji wake wa zamani na kumsajili mlinda lango Beno Kakolanya aliyeachwa na Yanga
Msemaji wa Yanga Dismas Ten kwa sasa ndiye anayetamba zaidi huko kwenye mitandao ya kijamii
Baadhi ya machapisho yake yamekuwa yakiwachanganya watani zake wa Simba hali inayopelekea wengine kufurumisha matusi
Moja ya machapisho aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram jana;
"Daaah kwa usajili huu unaofanywa na @yangasc naomba Serikali ifanye mabadiliko ya Viti upande ule wa kushoto, iweke vya chuma, vilivyopo sasa nahisi vitang’olewa sana msimu mpya ukianza
"Soma location uje sasa hivi ushuudie 'fundi wa mpira 'anasinya' (pichani anapitia mkataba kwanza) Kesho mchana tutabonyeza Play"



0 Comments