Windows

Bocco, Kagere tayari, bado Okwi



Safu ya ushambuliaji ya Simba msimu ujao itabaki kama ilivyokuwa msimu uliopita, zaidi itaongezewa nguvu kwa kusajiliwa nyota kadhaa kuchukua nafasi za ambao wataachwa/kutolewa kwa mkopo

Simba tayari imewaongezea mikataba nahodha John Bocco na Meddie Kagere ambao wote wamesaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja

Kagere yeye atakuwa na mkataba wa miaka mitatu kwani aliongeza miwili huku akiwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa awali

Anayesubiri kutambulishwa ni Mganda Emmanuel Okwi ambaye inaelezwa uongozi wa Simba umefanikiwa kumalizana nae na kumuongezea mkataba

Awali Okwi aligoma kusaini mkataba mpya akitaka mpaka michuano ya AFCON 2019 inayoanza Ijumaa huko Misri imalizike

Msimu uliomalizika Kagere, Bocco na Okwi waliifungia Simba mabao 54 kwenye ligi

Watatu hao kwa kushirikiana na nyota wengine wa Simba waliongoza moto wa mafanikio kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Kagere akifanikiwa kufunga mabao sita kwenye michuano hiyo ambayo Chama, Bocco, Okwi na Mkude nao walifunga

Post a Comment

0 Comments