Windows

Ofa zamiminika Msimbazi kumtaka Salamba



Licha ya kutokuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba, mshambuliaji Adam Salamba amezivutia timu nyingi ambapo uongozi wa timu hiyo umekiri kupokea ofa nyingi zinazomtaka mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kutoka Lipuli Fc

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema bado hawajafanya uamuzi kuhusu Salamba kwa kuwa bado wako kwenye mchakato wa usajili

"Ni kweli kuna timu zinamtaka Salamba lakini hatuwezi kuwajibu sasa kwa kuwa bado hatujakamilisha michakato yetu ya usajili," amesema

"Kuna mambo kadhaa tunapaswa kuyafanya kulingana na maelekezo ya mwalimu kabla ya kulifanyia kazi hilo"

"Nafahamu kuna wachezaji tutawaacha na wengine kuwatoa kwa mkopo lakini tuvute subira kidogo"

Inaelezwa klabu ya Polokwane City baada ya kushindwa kumnasa John Bocco aliyeongeza mkataba kunako klabu ya Simba, inamtaka Salamba kwa mkopo

Aidha klabu ya Nkana ya Zambia imetaka Salamba awe sehemu ya dili la mauziano ya Walter Bwalya anayewaniwa na Simba

Bwalya bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Nkana, timu hiyo imetaka ipewe fedha pamoja na Salamba

Pia inaelezwa kuna barua kutoka Ureno na Ubelgiji ambapo kuna timu zimemtaka aende akafanye majaribio

Post a Comment

0 Comments