Windows

Kennedy Wilson asaini miaka miwili Simba



Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa kati Kennedy Wilson kutoka klabu ya Singida United

Wilson ametambulishwa rasmi leo kuwa ingizo jipya kunako klabu ya Simba

Amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara

"Ingizo jipya kwenye kikosi cha Mabingwa, beki wa kati Kennedy Wilson Juma amesaini mkataba wa miaka miwili," imesema taarifa ya Simba

"Uwepo wa Kennedy kwenye kikosi kwa kushirikiana na mabeki wengine tulionao ni hakika safu yetu ya ulinzi itakuwa imara zaidi"



Post a Comment

0 Comments