Windows

Kennedy apania kufanya makubwa Simba



Simba leo imemtambulisha beki wake mpya Kennedy Wilson ambaye imemsajili kutoka klabu ya Singida United kwa mkataba wa miaka miwili

Wilson alikuwa nahodha wa Singida United, ametua Simba kuchukua nafasi ya beki Mganda Juuko Murshidi aliyemaliza mkataba na Simba

Beki huyo kisiki alikuwa miongoni mwa wachezaji walioitwa kuunda kikosi cha timu ya Taifa kabla ya kuondolewa katika mchujo uliobakisha wachezaji 23 ambao watashiriki michuano ya AFCON 2019 huko Misri

Baada ya kusaini mkataba wa kuwatumikia mabingwa hao wa nchi, Wilson amesema amefarijika kujiunga na Simba na atahakikisha anakuwa na mchango kwenye kikosi cha timu hiyo

Amesema hahofii ushindani wa namba kwani anafahamu ili aweze kupata nafasi lazima amshawishi kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems

"Simba ni timu kubwa, nitapambana na ushindani nitakaokutana nao ili niweze kumshawishi Mwalimu na hatimae kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza," amesema

Usajili wa beki huyo mwenye mwili mkubwa ni pendekezo la Aussems

Post a Comment

0 Comments