

Uongozi wa klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla pamoja na kamati ya Hamasa iliyoongozwa na Mh Athony Mavunde, kwa pamoja wanatoa shukrani za dhati kwa wanachama, mashabiki na wadau wa klabu ya Yanga kwa kufanikisha zoezi zima za uchangiaji fedha kwa ajili ya klabu ya Yanga
Aidha Dk Msolla na Mh Mavunde wanawapongeza sana wanachama, mashabiki na wadau wa Yanga wote kwa kujitoa kwa hali na mali katika michango na hatimaye kushiriki katika Tamasha la Kubwa Kuliko mwishoni mwa wiki
Pamoja na Shukrani na Pongezi hizo, Dk Msolla amewahakikishia Wanayanga wote kuwa michango yao ni ya thamani mno kwa klabu yao na kwamba uongozi utasimamia fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa
Pia amewataka kuendelea kujitoa kuiunga mkono klabu yao katika vipindi vyote ili kujijengea msingi imara wa kujitegemea kupitia kwa wanachama na mashabiki wake
"Tunawashukuru sana Wanayanga wote na wadau wengine, wakiwemo wale waliotupa udhamini wakati wa tukio letu la Kubwa Kuliko maana kwa pamoja wamefanikisha azma njema iliyopangwa na kamati ya Hamasa"
"Tutawalipa kwa kuhakikisha kile walichotoa kinasimamiwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa," amesema Dk Msolla
TIMU YA WANANCHI, WAWEKEZAJI NI WANANCHI



0 Comments