

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ataukabidhi uongozi wa klabu ya Yanga eneo la kujenga uwanja Kigamboni jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa, Juni 21 2019
Jana Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alimkabidhi Makonda nyaraka muhimu za utambulisho wa klabu kwa ajili ya zoezi hilo
Hata hivyo baadhi ya nyaraka zilikosekana hivyo zoezi la makabidhiano kuahirishwa hadi Ijumaa
Makonda amesema eneo tayari limepatikana kinachosubiriwa ni kukamilika kwa nyaraka hizo ili makabidhiano yafanyike
"Eneo limepatikana, na leo kama mlivyoona, nimekutana na viongozi wao ambao wamenikabidhi baadhi ya nyaraka, wamewasilisha asilimia 75 ya nyaraka ambazo wanatakiwa kuzitoa ili kuandikishwa kiwanja hicho," alisema Makonda jana baada ya kupokea nyaraka hizo kutoka kwa uongozi wa Yanga
Nyaraka ambazo hazikuwasilishwa ni katiba ya klabu pamoja na cheti cha usajili



0 Comments