

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda amekamilisha ahadi aliyoitoa siku ya Jumamosi kwenye Kubwa Kuliko baada ya leo kuongozana na viongozi wa Yanga mpaka Kigamboni na kuwaonyesha eneo ambalo atawakabidhi rasmi siku ya Ijumaa
"Leo tuko hapa Kigamboni nikiongoza na Mwenyekiti wa Yanga, Makamu, Kaimu Katibu Mkuu na viongozi wengine wa Yanga kuwaonyesha eneo ambalo niliwaahidi kuwapatia siku ya Jumamosi kwenye Harambee ya kuichangia timu hiyo," amesema Makonda
"Lengo la leo ni kuwaonyesha eneo, siku rasmi ya kuwakabidhi ni Ijumaa ambapo tutaweka jiwe la msingi na mashabiki wa Yanga tutakuwa nao hapa kuashiria mwanzo mpya wa klabu ya Yanga"
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema wanaweza kulitumia eneo hilo kujenga Academy ya Yanga ambayo itatumika kukuza vipaji vya wachezaji wadogo



0 Comments