

Uongozi wa Yanga unaendelea na maandalizi ya wiki ya Mwananchi ambayo wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo wataitumia kufanya shughuli mbalimbali za kijamii
Siku ya kilele cha wiki hiyo, Yanga itacheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kwenye uwanja wa Taifa, mchezo ambao utatumika kukitambulisha rasmi kikosi cha timu hiyo kilichosajiliwa
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema tukio hilo la kihistoria litafanyika mwezi wa nane tarehe ikiwa bado haijapangwa lakini ni kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu
Utaratibu wa aina hiyo umekuwa ukifanywa na watani zao Simba ambao wametangaza wiki yao itaanza August 01 na kuhitimishwa August 08
Wiki ya Mwananchi itakapoanza, wadau wa Yanga wameaswa kujitokeza kwa wingi kufanya shughuli za kijamii ili kudhihirisha msemo wa timu ya Wananchi



0 Comments