Windows

TAIFA STARS YAITOA JASHO MISRI, YAPIGWA 1-0

MCHEZO wa kiraļ¬ ki wa kimataifa kati ya Misri dhidi ya Taifa Stars, umemalizika kwa wenyeji Misri kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Katika mchezo huo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Borg El Arab uliopo Alexandria, bao la Misri lilifungwa dakika ya 64 kwa kichwa na Ahmed Elmohamady anayeitumikia Aston Villa ya England.

 

Kabla ya kuingia kwa bao hilo, Misri walionekana kuutawala mchezo huo tangu kuanza kipindi cha kwanza licha ya kipindi hicho kumalizika bila ya kufungana.

 

Mlinda mlango wa Taifa Stars, Aishi Manula, alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo mingi iliyoelekezwa langoni mwake muda wote wa mchezo huo. Safu ya ulinzi ya Taifa Stars, ilikuwa na kazi kubwa ya kuwazuia washambuliaji wa Misri waliokuwa wakiliandama lango lao wakiongozwa na kiungo mshambuliaji, Amr Warda.

Wakati Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike alipoona timu yake haitengenezi mashambulizi, dakika ya 62 alilazimika kumtoa John Bocco na kumuingiza Thomas Ulimwengu.

 

Dakika ya 75, Aggrey Moris alipata majeraha yaliyomfanya ashindwe kuendelea na mchezo, nafasi yake ikachukuliwa na Ally Mtoni, huku dakika tatu mbele, Farid Mussa akimpisha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, hata hivyo matokeo hayakubadilika.

 

Katika mchezo huo, staa wa Liverpool, Mohamed Salah hakucheza, kuanzia mwanzo wa mchezo alikuwa kwenye benchi la timu yake ya Misri huku muda mwingi akionekana akitabasamu na kucheka.

 

Dakika tano kabla ya mchezo kumalizika, aliinuka na kuingia vyumbani huku akiwapungia mkono mashabiki walioļ¬ ka uwanjani hapo.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa kiraļ¬ ki kwa Taifa Stars katika kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) ambayo inatarajiwa kuanza Juni 21, mwaka huu nchini humo.

 

Taifa Stars iliyopangwa Kundi C na timu za Kenya, Senegal na Algeria, itaanza kucheza na Senegal, kisha Kenya, halafu itamaliza hatua ya makundi kupambana na Algeria. Baada ya mchezo huo wa jana, Taifa Stars iliyopiga kambi nchini Misri tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, keshokutwa Jumapili itacheza mechi nyingine ya kiraļ¬ ki dhidi ya Zimbabwe.

 

TZ VS MISRI 0-1 SAMATTA, KOCHA Amunike Wafunguka Baada ya Kufungwa

The post TAIFA STARS YAITOA JASHO MISRI, YAPIGWA 1-0 appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments