UONGOZI wa timu ya Pamba SC ya jijini hapa, umetoa cheti cha shukrani kwa Gazeti la Championi ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango mkubwa wa gazeti hilo kwa msimu wa 2018/19 wakati Pamba ilipokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Akizungumza katika hafla ya kutoa vyeti iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini hapa, Aleem Alibhai ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Pamba SC, amesema kilichowasukuma kutoa cheti hicho kwa Championi ni kutokana na gazeti hilo kuwa na mchango mkubwa kwao.
“Sisi kama viongozi wa Pamba tumeamua kutoa cheti cha shukrani kwa Championi kama njia ya kutambua mchango wao kwetu kwa mafanikio tuliyopata kwa msimu uliomalizika wa Ligi Daraja la Kwanza,” alisema Alibhai na kuongeza.
“Kutokana na kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Championi na kupelekea timu yetu kukaa vichwani mwa watu, tunaamini lilitutangaza sana licha ya kushindwa kupanda daraja, lakini tunaamini msimu ujao pia tutapata sapoti yao na kufikia malengo.”
Pamba iliyokuwa Kundi B kwenye Ligi Daraja la Kwanza, ilimaliza nafasi ya pili na kupata nafasi ya kucheza mechi za mtoano dhidi ya Kagera, lakini ikapoteza kwa jumla ya mabao 2-0 katika mechi zote mbili za ugenini na nyumbani. [6/14,
PICHA: JOHNSON JAMES, MWANZA
RAIS TSHISEKEDI ALIVYOKAGUA BANDARI YA DSM
The post GAZETI LA CHAMPIONI LAPEWA TUZO MWANZA appeared first on Global Publishers.
0 Comments