MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameyashukuru Makampuni ya Global Group kutokana na kitendo cha kumtunuku tuzo mbili za heshima baada ya kuiwakilisha vyema Tanzania katika soka la kimataifa.
Samatta anayecheza soka la kulipwa katika Klabu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji, amewashukuru Global Group kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra yanayosomwa zaidi nchini, kutokana na kuthamini mchango wake katika kukuza soka la Tanzania kimataifa.
Mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars inayojiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, ametoa shukurani hizo baada ya kukabidhiwa tuzo wikiendi iliyopita alipofanya ziara maalum katika ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar.
Nyota huyo wa kimataifa mwenye rekodi za kutosha, alipewa tuzo ya kwanza ambayo ilikuwa ni kiatu cha dhahabu iliyokuwa na ujumbe ‘Mguu wa Dhahabu 2019 Mbwana Samatta’ wakati tuzo ya pili aliyopewa ilikuwa ikisomeka ‘Tuzo ya Mfano wa Kuigwa Mbwana Samatta 2019’.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Samatta alisema: “Mimi naweza kusema kitu kimoja, niwashukuru Global kwa zawadi hii ndogo ambayo wameamua kunipa, ni heshima kubwa sana kwangu japo kwa watu wengine inaweza kuonekana kama ndogo.”
TAZAMA MBWANA SAMATTA Alivyotunukiwa TUZO ya Heshima na GLOBAL GROUP
The post Samatta Aishukuru GlobalKwa Kumpa Tuzo Mbili – Video appeared first on Global Publishers.
0 Comments