MultiChoice Tanzania imetambulisha kampeni yao mpya ya Tupogo, ambayo ni maalumu kwa ajili ya mashindano ya Mataifa ya Afrika 2019 ‘AFCON’ nchini Misri kupitia + 255 Global Radio iliyopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Juni 21 ambapo Tanzania ipo kundi C ikiwa na timu nyingine ambazo ni Kenya, Senegal na Algeria.
Ofisa Masoko wa Multchoice Tanzania, Shumbana Walwa kupitia +255 Global Radio alisema wateja wanaotumia king’amuzi cha DSTV watawapa nafasi ya kuangalia mechi hizo kwa lugha ya Kiswahili, huku kivutio akiwa mtangazaji mpya wa michezo Salama Jabir ambaye atatangaza mpira kwa mara ya kwanza kwa Lugha ya Kiswahili.
Watangazaji wengine watakaotangaza michuano hiyo kupitia Super Sport ni pamoja na Ibrahim Masoud ‘Maestro’ , Maulid kitenge na Edo Kumwembe, amewaomba watanzania ambao hawatumii DSTV kujipatia king’amuzi ambacho kimeshaunganishwa na kifurushi cha Compact kwa 99,000/- ambacho kifurushi hicho kitakuonyesha mechi zote za michuano hiyo ya AFCON. Kwa wakazi wa Dar, piga namba hii 0659070707 utaletewa ulipo pamoja na huduma ya ufundi pia amesema kwa watazamaji wa kawaida wataweza kutazama mechi hizo 52 kupitia kifurushi cha DSTV bomba kwa lugha ya Kiswahili.
Pia mchambuzi mkongwe nchini, Masoud Maestro alisema kuwa wamejipanga vilivyo kuja kuwapa watanzania burudani ya uchambuzi mzuri pamoja na kufurahia Lugha adhimu ya Kiswahili.
PICHA: SWEETBERT LUKONGE, GPL
The post DSTV Yamtambulisha Salama Jabir, Kutangaza Kiswahili AFCON 2019 appeared first on Global Publishers.
0 Comments