Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ipo nchini Misri ikijiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON inayotarajia kutimua vumbi 21 Juni nchini humo.
Leo Juni 15, Stars itaingia dimbani katika mchezo wa pili wa majaribio dhidi ya Zimbabwe, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa El Sekka El Hadid jijini Cairo majira ya saa 2:00 usiku. Mchezo wa kwanza kufungwa na wenyeji timu ya taifa ya Misri kwa bao 1-0.
Stars ipo katika kundi C pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya, ambapo itacheza mchezo wake wa kwanza wa makundi Juni 23 dhidi ya Senegal.
Ikumbukwe Stars imepata nafasi hiyo baada ya miaka 39 kupita, ambapo mara ya mwisho kushiriki ni mashindano ya mwaka 1980 nchini Nigeria. Taifa Stars iliishia katika hatua ya makundi, ambapo safari hii inahitaji kujiandaa zaidi ili iweze kutengeneza historia mpya kwa kuvuka hatua ya makundi.
The post PASHAPASHA YA AFCON 2019: Taifa Stars vs Zimbabwe leo saa 2:00 Usiku appeared first on Global Publishers.
0 Comments