Yanga inaendelea na mchakato wa kuimarisha kikosi chake ambapo inaelezwa mpaka sasa idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa ni tisa
Kabla hajaondoka kuungana na kambi ya timu ya Taifa ya DR Congo, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisema kuwa amepanga kusajili nyota wapya 12 lakini akadokeza kuwa idadi hiyo inaweza kuzidi
Hivyo ni dhahiri zoezi la usajili la mabingwa hao wa kihistoria bado linaendelea
Ujio wa nyota wengi Yanga unamaanisha wachezaji wengi pia wataondoka
Mkuu wa Habari na Mawasiliano Yanga Dismas Ten amesema timu hiyo itafanya uamuzi kuhusu baadhi ya wachezaji baada ya kukamilisha usajli
Ten amesema lengo la Yanga ni kuboresha kikosi chake hivyo ni dhahiri wingi wa nyota wapya utapelekea baadhi ya nyota kuachwa na wengine kutolewa kwa mkopo
"Wapo baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika na hawatapewa mikataba mipya," amesema
"Pia wapo wachezaji ambao wanaweza kutolewa kwa mkopo kutegemea na uamuzi wa Mwalimu"
Bado uongozi wa Yanga haujaweka hadharani majina ya wachezaji ambao wameachwa na wale ambao wamesajiliwa
Hata hivyo timu zimetakiwa kutangaza mapema wachezaji waliochwa ili wapate muda wa kutosha kusaka timu nyingine
0 Comments