Windows

Niyonzima akaribishwe nyumbani au apotezewe?



Kiungo Haruna Niyonzima anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga baada ya kumaliza mkataba na Simba imefahamika

Tangu alipojiunga na Simba misimu miwili iliyopita, Niyonzima hakupata mafanikio kama aliyoyapata katika miaka yake mitano aliyoitumikia Yanga

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema hafahamu ukweli wa tetesi hizo kwa kuwa kazi ya usajili inasimamiwa na Kamati ya usajili

"Mimi sijui, lakini dirisha la usajili liko wazi hivyo kama Kamati ya usajili imezungumza na Niyonzima ni jambo la kawaida kwani wakati huu kamati inaweza kuzungumza na mchezaji yeyote ambaye wameona anaweza kuisaidia Yanga," amesema

Baada ya kukamilisha usajili wa nyota tisa wa kigeni, Yanga inaweza kuongeza mchezaji mmoja wa kigeni kuchukua nafasi ya Klaus Kindoki ambaye mkataba wake unasitishwa

Nyota wa kigeni waliosajiliwa na Yanga ni Lamine Moro (beki), Mustapha Suleyman (beki), Patrick Sibomana (winga), Issa Bigirimana(winga), Sadney Urikhob(winga/mshambuliaji), Maybin Kalengo(mshambuliaji) na Juma Balinya(mshambuliaji)

Wengine ni kiungo Papi Tshishimbi aliyeongeza mkataba na mlinda lango Farouq Shikalo ambaye mchakato wake wa usajili unaelezwa kuwa katika hatua za mwisho

Post a Comment

0 Comments