

Winga wa Lipuli Fc Miraji Athumani ni miongoni mwa wachezaji wanaohusishwa kusajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu ujao
Winga huyo aliyeifungia Lipuli Fc mabao saba msimu uliomalizika, leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram alibandika picha ambayo inaashiria jambo
Hata hivyo Simba imejiwekea utaratibu wa kutambulisha wachezaji wapya saa saba mchana
Hivyo kama tayari amesaini tutarajie utambulisho wake ndani ya wiki hii
Miraji ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wameitwa kikosi cha Stars kwa ajili ya michuano ya AFCON kabla ya jina lake kuondolewa kwenye mchujo wa mwisho uliobakisha wachezaji 23



0 Comments