Kiungo mshambuliaji mkongwe wa Yanga, Mrisho ngassa amesema kuwa ana ofa nyingi hivi sasa kutoka timu za hapa nchini na nje ya nchi ikiwemo Zambia na kama mipango ikikaa sawa basi ataondoka Jangwani.
Ngassa ameliambia Championi kuwa: “Nimepata taarifa kutoka uongozi juu ya kuniongezea mkataba mpya wa kubaki Yanga, lakini bado hatujakaa rasmi mezani kujadili mkataba huo, hivyo nawasubiria mabosi hao na kama tukishindwana basi nitaangalia sehemu nyingine ikiwemo kwenda Zambia.”
The post Ngassa Apata Ofa Kwenda Nje appeared first on Global Publishers.
0 Comments