

Msimu uliopita Heritier Makambo alii'ngarisha safu ya usambuliaji ya Yanga kwa kutupia mabao kambani
Baada ya Yanga kumuuza Mcongomani huyo klabu ya Horoya AC, wapo wanaoamini mabingwa hao wa kihistoria 'watapata tabu sana' kwa kumruhusu Makambo aondoke
Lakini wasichofahamu ni kuwa benchi la ufundi chini ya kocha Mwinyi Zahera liko makini na lilianza mchakato wa kumtafuta mbadala wake mapema sana na ndio maana wakatua Zambia klabu ya ZESCO kumsajili Maybin Kalengo, mshambuliaji ambaye yuko katika kipindi cha mafanikio ya maisha yake ya soka
Huyu Kalengo ni mshambuliaji aliyekamilika kwani ana kasi, nguvu, akili na macho ya kuliona lango
Uhodari wa Makambo ulikuwa zaidi kwenye mabao ya vichwa lakini huyu Kalengo anapiga hata nje ya 18
Pia hatakuwa peke yake kwani Yanga pia imemsajili kinara wa mabao ligi kuu ya Uganda msimu uliomalizika Juma Balinya
Balinya aliweka rekodi huko Uganda akiitumikia Polisi Fc kwa kufunga mabao 19 katika mechi 24 tu, huu ni wastani wa juu sana wa 'kutupia kambani'
Wakali hawa hawatakuwa peke yao, watasaidiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Namibia Sadney Urikhob



0 Comments