


KIPA mpya wa Simba, Benno Kakolanya, amesema yupo tayari kuanzia benchi katika kikosi chake hicho kwani hata alivyokuwa Yanga, ilikuwa hivyo lakini hatimaye alipata nafasi.
Kakolanya amejiunga na Simba akitokea Yanga, baada ya kuvunjwa mkataba wake, kwa madai ya kutofautiana na kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera aliyekuwa akimshtumu kwa utovu wa nidhamu.
Kakolanya alisusa kuitumikia Yanga akishinikiza kulipwa fedha zake za mshahara na madai mengineyo, kitendo kilichomchukiza Zahera, ukizingatia si pekee aliyekuwa akidai.
Akizungumza na BINGWA jana, Kakolanya alisema hana hofu ya namba ndani katika cha Simba akiamini Wekundu wa Msimbazi wanamkubali ndio maana wamemsajili.
“Hata nilipoanza kukitumikia kikosi cha Yanga, sikupangwa moja kwa moja, nilianzia benchi, lakini baadaye nilipata nafasi ya kucheza,” alisema kipa huyo.



0 Comments