Windows

JASHO NA DAMU



LIVERPOOL wanataka kulichukua kombe kwa mara ya sita kama walivyofanya mwaka 2005, baada ya kuifunga AC Milan kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 3-2.

Hata hivyo, wapinzani wao Tottenahm wana ndoto ya kulibeba kombe hilo na kuishangaza Liverpool kwenye mtanange huo wa kukata na shoka.

Liverpool walitinga fainali baada ya kuichapa Barcelona huku Totteham wakiwang’oa Manchester City kwa faida ya mabao ya ugenini.

Rekodi za mchezo wa leo utakuwa wa tatu msimu huu kwa timu hizo kuvaana huku Liverpool ikishinda michezo yote katika mechi za Ligi Kuu England (EPL).

Klopp vs Pochettino: Msimu huu utakuwa wa mara ya kwanza kwa makocha wa Ligi Kuu England kukutana kwenye fainali hii.

“Kucheza fainali ni ndoto ya kila mchezaji kwenye mashindano haya najivunia msimu huu kufika hatua hii na hatuna hofu tupo tayari kwa mechi hii,” alisema Pochettino.

Aidha, kwa upande wa Klopp anaimani wataifunga Tottenham na kufuta kumbukumbu mbaya ya fainali ya msimu uliopita dhidi ya Real Madrid.

“Nina timu nzuri msimu huu sitaki kukumbuka yaliyotokea Kiev, tumepata nafasi nyingine na nitasikitika endapo tutapoteza kwa mara nyingine tena,” alisema Klopp.

Tottenham itamkosa kiungo Harry Winks huku Harry Kane akitarajiwa kuanza kwenye mechi hiyo baada ya kupona majeraha.

Liverpool kwa upande wao watakosa huduma ya kiungo wao, Naby Keita, huku Roberto Firmino akiwa fiti kwa ajili ya kuivaa Tottenham leo.

Kikosi cha Tottenham: Lloris, Trippier, Alderweireld, Vertonghen, Rose, Sissoko, Alli, Eriksen, Moura, Son na Kane.

Kikosi cha Liverpool: Alisson, Alexander-Arnold, Matip, Van Dijk, Robertson, Fabinho, Henderson, Wijnaldum, Mane, Salah na Firmino.

Post a Comment

0 Comments