NAHODHA wa Real Madrid, Sergio Ramos, amesema atabaki katika klabu hiyo na malengo yake ni kuzeeka akiwa na timu hiyo.
Awali Rais wa klabu hiyo, Frolentino Perez, alikiri kuwa beki huyo aliomba nafasi ya kuondoka ili kujiunga na Ligi Kuu ya China.
Hata hivyo, ombi hilo lilitupiwa mbali na Perez na kudai hawapo tayari kumwachia huru msimu ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari Ramos mwenye umri wa mika 33, alisema maisha yake yote ataendelea kuwepo kwenye klabu hiyo.
“Nina mawasiliano mazuri na Perez na hivi karibuni nitaongeza kandarasi mpya. Nataka kuweka wazi kuwa nitazeeka kwenye klabu hii na sitaenda popote,” alisema Ramos.
Ramos alicheza mechi 42 katika mashindano yote ambayo walicheza, huku akiifungia timu hiyo mabao 11 licha ya kuwa na hali mbaya msimu huu.
0 Comments