Windows

Ujio wa Shikalo wamuweka njiapanda Kindoki


Yanga tayari imemsajili mlinda lango Farouq Shikalo kutoka Bandari Fc ya Kenya kwa mkataba wa miaka miwili

Moja ya sharti lililo kwenye mkataba wake, ni 'nyanda' huyo wa Harambee Stars kuwa kipa namba moja



Lakini Yanga imedhamiria kumaliza kabisa hofu eneo la ulinzi wa lango ambapo inaelezwa iko mbioni kukamilisha usajili wa mlinda lango wa Mbao Fc Metacha Mnata

Metacha tayari yuko jijini Dar es salaam kujiunga na kambi ya timu ya Taifa na inaelezwa viongozi wa Yanga wanataka kukamilisha usajili wake kabla hajaingia kambini leo



Kama Yanga itamsajili Metacha huenda mlinda lango mmoja kati Klaus Kindoki au Ramadhani Kabwili ataachwa

Aliye hatarini zaidi ni Kindoki kwani haitarajiwi Yanga kuwa na walinda lango wawili wa Kimataifa

Ujio wa Shikalo unaweza kumuondoa Kindoki ili nafasi yake aongezwe mchezaji wa ndani

Kabwili anaweza kuongezewa mkataba licha ya kuwa mazungumzo ya mkataba mpya bado hayajaanza

Post a Comment

0 Comments