Windows

Iran yaonywa tena dhidi ya Marekani


Mshauri mkuu wa usalama wa Marekani John Bolton, ameonya Iran, kutochukulia hatua ya Rais Donald Trump kusitisha shambulizi la kulipiza kisasi dhidi yake kama unyonge au udhaifu.

Israel na nchi za Ghuba zinaichukulia Iran kuwa kitisho chao kikubwa na hatua ya Trump kusitisha shambulizi dhidi yao, imeibua maswali kuhusu uwezo wa Marekani wa kushambulia Iran.

Wiki iliyopita Iran, ilidungua ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani na Rais Trump akaapa kulipiza kisasi kabla ya kusitisha tena hatua hiyo.

Post a Comment

0 Comments