Msanii nyota wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee anajiandaa kuachia E.P yake (nyimbo chache zinazounganishwa pamoja) ambayo ameiita Expensive.
Katika uthibitisho wa hilo, ametuonesha Cover art ya EP hiyo ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni. Habari njema ni kwamba ndani ya EP hiyo pia Vanessa ana Collabo na mdogo wake Mimi Mars.
Tayari Mimi Mars alithibitisha ujio wa Collabo hiyo akiwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio hapa nchini mwezi mei mwaka huu na pia alisema Collabo hiyo ndiyo iliyobeba jina la EP hiyo.
Vanessa Mdee atakuwa msanii wa pili kutoka kwenye Bongo Fleva kwa mwaka huu kuachia EP baada ya Harmonize aliyeachia ya kwake inayokwenda kwa jina la Afro Bongo.
0 Comments