Windows

Jean Pierre Bemba arejea DR Congo


Kiongozi wa upinzani na Mbabe wa Kivita nchini DR Congo, Jean-Pierre Bemba, aliekuwa amezuiliwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu amerejea mjini Kinshasa hapo jana ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha chini ya mwaka kurejea nchini humo .

Bemba, aliwasili katika uwanja wa ndege wa Ndjili akiwa katika ndege binafsi na kupokelewa na mgombea wa kiti cha u-Rais alieshindwa katika uchaguzi Martin Fayulu.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Didier Reynders ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa kurejea kwa Jean Pierre Bemba na viongozi wengine wa upinzani ni hatua muhimu nchini humo.

Post a Comment

0 Comments