Windows

Global FC Kuwavaa Bongo Fleva


Timu ya Global FC inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Wasanii wa Bongo Fleva, Bongo Fleva Fc.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Ijumaa ya wiki ijayo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe, Bagamoyo.

Akizungumzia mchezo huo, nahodha wa Bongo Fleva, Rich One alisema maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya mchezo huo.

“Maandalizi yanakwenda vizuri ya mchezo wetu na kikosi chetu kina morali ya juu kuhakikisha tunapata ushindi

” Kikosi chetu kinatarajiwa kuongozwa na wasanii wakubwa na maarufu ambao ni TID, Stamina, Papii Kocha, M2 The P na wengine wengi, alisema Rich One.

Kwa upande wa nahodha wa Global FC, Wilbert Molandi ‘Momo’ anayemudu kucheza nafasi ya Kiungo naye alisema kuwa” Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kikubwa katika mchezo huo wanahitaji ushindi pekee.

“Tunatarajia kushusha mziki mzima katika mchezo huo kwa maana ya wachezaji wetu wote akiwemo Ally (Saleh) na Nkini (Philip).

Na Mwandishi Wetu

The post Global FC Kuwavaa Bongo Fleva appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments