Windows

Caf Yamruhusu Kessy Kuivaa Senegal

UONGOZI wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limemruhusu beki wa Taifa Stars, Hassan Kessy, kucheza mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) dhidi ya Senegal, utakaofanyika leo Jumapili kwenye Uwanja wa 30 June Cairo, Misri.

 

Uamuzi huo wa Caf, umekuja baada ya kuenea kwa taarifa kwamba, Kessy hawezi kucheza mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

 

Taarifa iliyotumwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenda kwa vyombo vya habari jana Ijumaa, inasema kuwa: “Baada ya Caf kujiridhisha kuwa, Hassan Kessy hana kadi mbili za njano ambazo zinasemekana zingemfanya asicheze mchezo huo, zilishaisha katika mchezo namba 101 ambao ulikuwa ni dhidi Cape Verde hapa nyumbani.”

“Kutokana na taarifa hiyo, Kocha Emmanuel Amunike, anaweza kumtumia Kessy katika mchezo huo wa kwanza wa Afcon bila ya tatizo lolote kama atakuwa yupo kwenye programu yake.”

 

Kessy alipata kadi mbili za njano katika michezo miwili ya ugenini dhidi ya Uganda na Cape Verde na kumfanya aukose mchezo mmoja wa marudiano dhidi ya Cape Verde uliochezwa Oktoba 16, mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa, ambapo Taifa Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

The post Caf Yamruhusu Kessy Kuivaa Senegal appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments