Windows

Gadiel Michael aongeza mkataba Yanga


Beki wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael ataendelea kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu, imefahamika
Gadiel aliyekuwa akitajwa kuwaniwa na Simba, yuko kwenye kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadae mwezi huu nchini Misri
Ni miongoni mwa wachezaji walion'gara katika kikosi cha Yanga kilichomaliza nafasi ya pili ligi kuu ya Tanzania Bara msimu uliomalizika
Alisajiliwa na Yanga miaka miwili iliyopita akitokea Azam Fc, usajili wake ukiibua utata mkubwa baada ya Azam Fc awali kumuwekea ngumu kabla ya kumruhusu baadae

Post a Comment

0 Comments