Windows

Chirwa aipandisha ndege Azam

MSHAMBULIAJI Obrey Chirwa wa Azam ameibuka kuwa shujaa katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Lipuli baada ya kuifungia timu hiyo goli la ushindi, mechi hiyo imechezwa uwanja wa Ilulu, Lindi.\

Azam imeifunga Lipuli bao 1-0 na ushindi huo umewapa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao.
Katika kipindi cha pili Azam ilibadilika na kuanza kucheza soka maridadi katika kuhakikisha kwamba wanapata goli.
Dakika 62 Azam ilifanya mabadiliko ya kumtoa Mudathir Yahya na kuingia Frank Domayo, Mudathir alionekana kushindwa kuendelea kutokana na kupata majeraha.
Mabadiliko hayo yaliwafanya Azam kuzidi kutawala katika eneo la kiungo katika ukabaji na kushambulia tofauti na ambvyo likuwa katika kipindi cha kwanza kwa timu zote kuwezana kwenye eneo hilo.
Dakika 64 Azam ilipata goli kupitia kwa Chirwa ambaye alipokea pasi kutoka kwa kipa Razack Abarola aliyepiga shuti kutoka golini na kukutana mshambuliaji Chirwa ambaye alimzidi nguvu beki Haruna Shamte na kuutuliza mpira chini kisha alipiga shuti ambalo lilienda moja kwa moja wavuni.
Goli hilo liliwaongezea morali ya kupambana wachezaji wa lipuli lakini hata hivyo walikuwa wanakutana na ugumu kupitia ulinzi wa mabeki Yakub Mohammed, Daniel Amoah na Aggrey Morris.
Kukosekana kwa Ally Mtoni katika kikosi cha Lipuli, kuliwafanya Azam kupitia mshambuliaji wake Chirwa kutamba mbele ya Novatus Lufunga na Shamte.
Lipuli ilifanya mabadiliko dakika 71 kwa kumtoa Daruesh Saliboko na kuingia Silvester Mganga na Zawadi Mauya alitoka nafasi yake ilichukuliwa na Seif Kalie ili kwenda kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji.
Hata hivyo mabadiliko hayo kwa Lipuli hayakuweza kubadilisha matokeo yoyote katika mchezo huo.


Post a Comment

0 Comments