Windows

Ninja: Hata Simba nipo tayari kucheza

BEKI wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' amesema mkataba wake umemalizika kwa sasa yupo huru kuzungumza na timu yoyote ikiwemo Simba kama watahitaji huduma yake

Ninja alikuwa kati ya mabeki tegemeo ndani ya kikosi cha kwanza cha kocha Mwinyi Zahera alisema bado viongozi wa Yanga hawajakaa naye mezani kuanza mazungumzo mapya lakini alidai soka kwake ni kazi hivyo anafungua milango kufanya kazi na timu yoyote.

"Soka ni kazi yangu sawa na mkulima ambaye hajagui jembe, kama Yanga wataona nafaa kuendelea nao sawa pia ikitokea timu nyingine yakufanya nayo kazi pia sawa ikiwemo Simba.

" Msimu huu kwangu ulikuwa wa mafunzo mengi ambayo yamenifumbua macho kujua nini natakiwa kufanya kwenye ulimwengu wa kazi hii, siwezi kujifungia vioo na timu za ndani zikija za nje pia nitakuwa tayari kuondoka"alisema.
Ninja alisema hatakuwa na shukrani kama hatakiri kwamba Yanga imemsaidia kutambulisha kipaji chake kwa madai tofauti na alivyokuwa ametoka Taifa Jang'ombe ya Zanzibar.
"Yanga imefanya nijulikane kwa umbali mrefu kwa maana ya kazi yangu ingawa malengo yangu hayajatimia ya kutamani kuvaa medali lakini ndio changamoto za kazi, lakini haina maana kwamba ndio nijifungie vyoo kushindwa kufanya kazi na wengine" alisema.
Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika Yanga ni Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Haruna Moshi 'Boban', Haji Mwinyi na wengineo.


Post a Comment

0 Comments