Windows

BAKHRESSA WANOGESHA NDONDO CUP

Mwenyekiti wa Ndondo Cup, Shafii Dauda (kushoto), akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kupokea udhamini mpya wa mashindano hayo kutoka katika kampuni ya Bakheressa Group.  Kulia ni Msimazi Mkuu wa Magomeni Ice Cream Center, Ibrahim Wasome.

 

KAMPUNI ya Bakhressa nchini imenogesha Ndondo Cup kwa kudhamini michuano hiyo inayotarajiwa kuendelea keshokutwa ambayo imefikia hatua ya 32 bora.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Ndanda Cup, Shafii Dauda, alisema kuwa Bakhressa imewawezesha katika udhamini huo kwa kuwapatia vinywaji na bidhaa nyinyine zitokanazo na kampuni hiyo.

Wasome akizungumza na waandishi wa habari

“Kuelekea katika hatua hii ya makundi ambayo ufunguzi wake utafanyika Uwanja wa Bandari,  Tandika, Mwembe-Yanga, jijini Dar es Salaam Julai 7, mwaka huu, Kampuni ya Bakhressa imetuwezesha katika udhamini ambapo mashabiki watapata vinywaji kupitia kiingilio cha shilingi 2,000 kwa maana unapotoa kiingilio utapewa tiketi pamoja na kinywaji utakachochagua, ” alisema Dauda.

Naye Meneja wa Magomeni Ice Cream, Ibrahim Wasome,  alisema: “Michuano hii imekuwa na umaarufu mkubwa ikiwemo kutoa wachezaji ambao hivi sasa wanafanya vizuri, kwa hiyo nawakaribisha sana mashabiki.   Mbali na kinywaji utakachochagua kwenye kiingilio,  kinywaji rasmi kitakachotumika kwenye michuano hii kitauzwa kwa bei ya punguzo.”

Na Mwandishi Wetu

The post BAKHRESSA WANOGESHA NDONDO CUP appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments