

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuondoka nchini usiku wa leo kuelekea DR Congo kuungana na timu ya Taifa, yeye akiwa kocha Msaidizi
DR Congo itashiriki fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwezi ujao nchini Misri
Congo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Misri, Zimbabwe na Uganda
Zahera amesema timu hiyo inaelekea Hispania kuweka kambi, ambapo watangia kambini May 31
Tanzania pia itashiriki fainali za michuano hiyo ikiwa imepangwa kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Kenya
Baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, Zahera ameahidi kutangaza majina ya wachezaji wapya nane aliowasajili Yanga pamoja na wachezaji wanaoachwa na timu hiyo



0 Comments