

Kiungo Ibrahim Ajib alikuwa amepata nafasi nzuri ya kwenda kusakata kabumbu katika klabu ya TP Mazembe yenye historia ya kuuza wachezaji Ulaya
Mbwana Samatta nahodha wa Stars ni mfano mzuri wa mchezaji anayewika sasa barani Ulaya ambaye alipikwa katika klabu ya TP Mazembe
Hata hivyo Ajib amekubali siasa za Simba na Yanga zimkwamishe, hakika baadae anaweza kuja kujutia uamuzi wa kuikacha TP Mazembe ili abaki Tanzania
Ni jambo la kutia moyo kuona uongozi wa Yanga ulimpa baraka zote kwenda TP Mazembe licha ya mchezaji huyo kuwa na umuhimu katika kikosi cha timu hiyo
Hata hivyo uamuzi wake wa kuiacha 'dili' hiyo umewashangaza wengi
Inaelezwa Ajib tayari alishachukua fedha Simba 'kishika uchumba' ili aweze kujiunga na timu hiyo pindi mkataba wake utakapomalizika
Wapo wanaosema Ajib kujiunga Simba ni sawa kwa sababu kwa sasa Simba ni timu kubwa sawa na TP Mazembe!
Mawazo haya ndio yanayochangia kulifanya soka letu lidumae kwani mafanikio ya msimu mmoja tu basi tunadhani tumeshafika mwisho wa safaricut
TP Mazembe ni taasisi kubwa sana, wana uwanja wao, wana vifaa vya kisasa vya mazoezi, Mazembe wana shule za kukuzia vipaji
Ni moja ya timu chache sana barani Afrika ambazo zinamiliki usafiri binafsi wa Ndege
TP Mazembe iko mbali sana, wana mazingira mazuri ya kumfanya mchezaji awe bora zaidi na kumuongezea thamani
Ajib amekubali siasa za Yanga na Simba zimpotezee nafasi adimu ya kwenda kucheza katika moja ya vilabu vyenye histoaria na mafanikio makubwa barani Afrika
Amekubali kupoteza nafasi adimu ambayo pengine ingempa tiketi ya kwenda kusakata kabumbu barani Ulaya
TP Mazembe walimtaka Ajib baada ya kumuona ana kipaji, bila shaka asingekaa muda mrefu katika klabu hiyo ambayo imejipambanua kuwa daraja la wachezaji kuvuka kuelekea Ulaya



0 Comments