

Kikosi cha Yanga leo kinashuka kwenye uwanja wa Uhuru kukamilisha msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2018/19 kwa kumenyana na Azam Fc
Yanga inayonolewa na kocha Mwinyi Zahera, imekuwa kikijifua uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo wa heshima
Tayari imejihakikishia kumaliza nafasi ya pili hivyo matokeo yoyote ya mchezo huo hayatabadili nafasi yao kwenye msimamo wa ligi
Hata hivyo uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa wanataka kumaliza msimu vizuri kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Azam Fc ambayo waliifunga bao 1-0 katika mchezo wa duru ya kwanza
Yanga itawakosa nyota wake kadhaa ambao ni wagonjwa
Mchezo dhidi ya Azam Fc utakuwa wa mwisho kwa baadhi ya wachezaji kwani baada ya mchezo huo, Yanga itaweka hadharani majina ya wachezaji wanaotemwa
Aidha mshambuliaji Heritier Makambo atapata nafasi nyingine ya kuwaaga mashabiki wa Yanga, huo ukiwa ni mchezo wake wa mwisho kabla ya kutimkia Horoya AC



0 Comments