

Mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC) umemalizika kwa timu ya Yanga SC kuchapwa goli 2-0 na Lipuli FC katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Lipuli FC walipata goli la kwanza kupitia Paul Nonga dakika ya 29 baada ya piga nikupige kwenye lango la Yanga.
Miraj Athuman aliandika bao la pili kwa Lipuli FC dakika 39 baada ya mabeki wa Yanga kufanya makosa kama ya awali kuzembea kuokoa mpira.
Kwa matokeo hayo Lipuli FC moja moja inafuzu kucheza hatua ya fainali ambalo watacheza na Azam FC. Utakumbuka msindi wa kombe hilo ndiye anaenda kuiwakilisha nchi kwenye Michuano ya CAF ya shirikisho barani Afrika.




0 Comments