Windows

Kocha wa Yanga SC afunguka kuhusu Lipuli




Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameeleza kuwa atatumia dakika 15 kumaliza mchezo wa leo dhidi ya Lipuli utakaochezwa Uwanja wa Samora ikiwa ni hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho.

Zahera amesema kuwa wanaitambua Lipuli namna inavyopambana kutafuta matokeo hivyo ili kupata ushindi ni lazima wapambane kushinda mapema kabla ya kwenda mapumziko.

"Namna ambavyo Lipuli wanacheza pamoja na kikosi changu kilivyo ni lazima tupambane kupata matokeo mapema, nimewaambia wachezaji wangu ndani ya dakika 15 mpaka 20 wanatakiwa wafanye juhudi kutafuta matokeo kisha tukienda mapumziko tutakuwa na jambo lingine la kufanya.

"Kama mchezaji atashindwa kufuaa maelekezo ndani ya dakika hizo sitaona taabu kumtoa ila ninaamini tupambana kwani mchezo wetu wa mwisho wa ligi tulipoteza na niliwapongeza wachezaji kwani walipambana licha ya kupoteza," amesema Zahera.

Mshindi wa mchezo wa leo atatinga hatua ya fainali ambapo atacheza na Azam FC ambao wao walishinda mbele ya KMC ushindi wa bao 1-0.

Post a Comment

0 Comments