

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika hafla ya tuzo za Simba inayofahamika kama Mo Simba Awards itakayofanyika keshokutwa Alhamisi, May 30 2019 Kilimanjaro Hotel jijini Dar es salaam
Uongozi wa Simba umesema maandalizi kuelekea tuzo hizo zilizoingia katika msimu wa pili yamekamilika
Baada ya kukabidhiwa ubingwa mkoani Morogoro leo, kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam kesho tayari kwa tukio hilo la kihistoria



0 Comments