Windows

Zahera amkana Ndemla, ampotezea Ajib



Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla sio miongoni mwa wachezaji anaowawania kuwasajili

Akizungumza leo baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc uliomalizika kwa Yanga kufungwa mabao 2-0, Zahera amesema Ndemla hayumo katika orodha ya wachezaji wake wapya

"Nani, Ndemla yule mchezaji wa Simba, hayumo kwenye karatasi yangu", amesema Zahera

Katika hatua nyingine, Zahera ameeleza kushangazwa na taarifa za kukwama kwa usajili wa Ibrahim Ajib kuelekea TP Mazembe

"Mimi sifahamu kama usajili wake umekwama. Baada ya kupigiwa simu na viungozi wa TP Mazembe nilizungumza na Ajib na akaniambia angependa kwenda kucheza Mazembe"

"Sijui nini kimetokea, nikitoka hapa nitampigia kiongozi wa TP Mazembe anifahamishe," amesemacut

Sibomana asaini miaka miwili

Taarifa za uhakika Yanga imekamilisha usajili wa Patrick Sibomana, winga kutoka Mukura Victory ya Rwanda

Inaelezwa Sibomana amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria



Wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamu taarifa za usajili wa timu hiyo ambapo Zahera aliahidi kuweka kila kitu hadharani baada ya mchezo wa leo dhidi ya Azam Fc

Post a Comment

0 Comments