

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Simba, Abas Abdalah amesema kuwa kikosi kipo imara na wanapambana kupata matokeo.
"Kwa sasa tupo vizuri na tuna kazi ngumu ya kufanya kwenye ligi kutokana na malengo ambayo tumejiwekea, ligi ni ngumu hilo lipo wazi ila tunapambana katika michezo yetu iliyobaki.
"Hakuna mchezaji ambaye ni mgonjwa kwetu zaidi ya Shomari Kapombe ambaye naye ameanza mazoezi wengine wote wapo fiti kwa ajili ya kupambana," amesema.
Simba kesho inashuka uwanjani kumenyana na Mbeya City mchezo utakaochezwa uwanja wa Sokoine.



0 Comments