Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku ameonyesha wasiwasi wake wa kubaki kwenye timu hiyo baada ya kusema hana uhakika wa kuwa hapo msimu ujao.
Mshambuliaji huyo ameshindwa kufanya vizuri kwenye kikosi cha Manchester United msimu huu na amekuwa akichukiwa sana na mashabiki wa timu hiyo.
Hivi karibuni taarifa zilitoka kuwa anawindwa na timu kadhaa kubwa ikiwemo Juventus na Inter Milan zote za Italia.
Wiki iliyopita alinukuliwa akisema kuwa atafurahi kama siku moja atacheza kwenye Ligi Kuu ya Italia, Serie A.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 bado ana mkataba wa miaka mitatu na United.
"Mimi sijui kama nitakuwa hapa msimu ujao, lakini ieleweke kuwa sipo hapa kufuatilia tetesi zinasemaje.
"Naamini kuwa bado msimu wa ligi haujamalizika na kuna kazi kubwa sana, natakiwa kuifanya ndiyo naweza kuwaza mambo mengine."
Lukaku kwenye michuano yote msimu huu amefanikiwa kucheza michezo 45 amefunga mabao 15 na kufanikiwa kutoa pasi nne za mabao.
0 Comments