


KUNGO mshambuliaji wa Barcelona, Ivan Rakitic, ameuambia uongozi wa klabu hiyo kumsajili nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, ambaye alitangaza kuondoka.
Rakitic aliweka wazi kuwa ni jambo la furaha kwa klabu hiyo kumnunua mchezaji huyo ghali kwa sasa.
“Ni mchezaji wa kiwango kikubwa duniani, na tutafurahi akijiunga pamoja na sisi. Ameshinda vikombe vingi na atakuwa usajili mzuri,” alisema Rakitic
Tayari miamba hao wamefanikiwa kunasa saini ya kiungo wa Ajax, Frenkie de Jong, ambaye atajiunga nao msimu ujao.
Wakati huo huo Rakitic amekanusha uvumi uliokuwa ukimuhusisha kuwa ataondoka Barcelona na kujiunga na Inter Milan.



0 Comments