


BILIONEA Roman Abramovich anaripotiwa kupoteza zaidi ya pauni milioni 92.9 sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 270.2 za Kitanzania kwa kuwalipa makocha aliowafukuza tangu aanze kuimiliki klabu ya Chelsea mwaka 2003.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, tangu kibopa huyo ainunue Blues, kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wake, Ken Bates, tayari makocha 11 wameshakuja na kuondoka chini ya utawala wa bilionea huyo wa kirusi akiwamo, Jose Mourinho aliyefukuzwa mara mbili.
Gazeti hilo linaeleza kuwa na huenda hivi karibuni akawa kocha wa 12, baada ya Maurizio Sarri,kutishia kuondoka na huku klabu ya Juventus ikiripotiwa kuwa tayari kumpeleka mjini Turin ili aweze kumrithi aliyekuwa wa kwao, Massimiliano Allegri.
Taarifa za gazeti hilo zinaeleza kuwa kocha huyo wa zamani wa Napoli, amepewa kibarua cha kuhakikisha anatwaa ubingwa wa Ligi ya Europa ili aweze kujihakikishia hatima ya kibarua chake kwenye klabu hiyo ya Bridge.
Lilieleza kocha wa mwisho kufukuzwa Stamford Bridge alikuwa ni Antonio Conte, ambaye klabu hiyo ya Magharibi mwa jiji la London, imeagizwa kumlipa kitita cha pauni milioni 9.
Gazeti hilo linadai wa kwanza kukumbana na jeurihiyo ya fedha ya Abramovich alikuwa ni Claudio Ranieri aliyelipwa pauni milioni 6, baada ya kuifundisha timu hiyo msimu mmoja kabla ya kuteuliwa Mourinho.
Hata hivyo mwaka 2007 ‘Special One’ na benchi lake la ufundi wakapewa pauni milioni 23.1, baada ya kuimliwa na aliyewafuatia Avram Grant akalipwa pauni milioni 5.2, baada ya kufukuzwa Mei 2008, siku chache baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wengine ambao walimkamua bilionea huyo ni Luiz Felipe Scolari, aliyepewakitta cha pauni milioni 12.6, baada ya kufukuzwa ikiwa nitakribani miezi saba tangu akabidhiwe tiu hiyo, Carlo Ancelotti aliyetimliwa kwaharaka baada ya kupoteza mechi ya mwisho dhidi ya Everton msimu wa 2010/11 naye akalipwa pauni milioni 6 na Andre Villas-Boas ambaye alishindwa kuelewana na Abramovich, baada ya kuwasili katika klabu hiyo akitokea FC Porto na hivyo kufungashiwa virago Machi 2012 na akalipwa pauni milioni 12.
Makocha wengine waliotimliwa na bosi huyo na fedha walizoondoka nazo kwenye mabano ni kama ifuatavyo, Roberto Di Matteo (pauni mil.10.7, Rafa Benitez (Hakulipwa), Mourinho (Pauni mil 8.3, Guus Hiddink (Hakulipwa) na endapo atamfukuza Sarri kiasihicho kinaweza kufikia pauni milioni 100



0 Comments