Baada ya utawala wa misimu mitatu mfululizo ya UEFA Champions League na Real Madrid, msimu wa 2018/2019 tutapata Bingwa mpya wa michuano hiyo itakayokuwa inazikutanisha timu za Liverpool na Tottenham Hotspurs zote za England zikikipiga June 1 2019 katika jiji la Madrid katika uwanja wa Wanda Metropolitano.
Game hiyo kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ndio ataingia uwanjani na presha zaidi kutokana na kuwa atakuwa anacheza fainali ya tatu ya UEFA Champions League pasipokuchukua kama atapoteza baada ya msimu uliopita kufungwa na Real Madrid na aliwahi kupoteza akiwa na Borussia Dortmund (), hivyo kwa yeye hatua ya fainali sio mafanikio kwake tofautisha na Pochettino.
Mauricio Pochettino anaingia bila presha katika mchezo tayari ikidaiwa kuwa amefikia lengo na target ya club yake, kwani kwa timu kama Tottenham kufika fainali timu ya UEFA Champions League ni mafanikio makubwa sana kwake, kwani kabla ya msimu huu waliwahi kufika hatua za juu zaidi katika michuano hiyo ni nusu fainali msimu wa 1961/1962 hivyo hayo ni mafanikio.
Kuelekea mchezo huo kocha wa zamani wa vilabu vya Man United na Chelsea Jose Mourinho ametoa kauli inayoashiria kuwa Klopp atakuwa na presha zaidi katika mchezo huo “Kama Jurgen Klopp hatoshinda, kiukweli kupoteza fainali tatu za Champions League, hiyo itakuwa ngumu sana”
0 Comments