Windows

Liverpool bado inamnyima usingizi Lionel Messi




Moja kati ya game za kushangaza zaidi katika michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 ni game za nusu fainali za UEFA Champions League kati ya FC Barcelona dhidi ya Liverpool zilizochezwa nyumbani na ugenini.

FC Barcelona katika game hiyo walipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kutokana na mchezo wao wa kwanza Nou Camp kumaliza kwa ushindi wa magoli 3-0, hivyo walienda Anfield kutafuta sare au wapate goli moja ili waweze kumtoa Liverpool ila mambo yakawa tofauti na kujikuta wakifungwa magoli 4-0 na kutolewa kwa tofauti ya goli moja.



Lionel Messi ambaye ni nahodha wa Barcelona ameaumizwa na kipigo hicho na hata alipoulizwa anajisikiaje kutwaa kiatu cha sita cha dhahabu cha michuano ya Ulaya akifunga magoli 12 tofauti ya magoli manne na wanaomfuatia, alijibu kuwa furaha yake haijakamilika kutokana na kuondolewa katika michuano hiyo na hafikiri tuzo binafsi.

“Kiukweli sifikiri hata kidogo kiatu cha dhahabu cha michuano ya Ulaya, hakipo akilini mwangu kabisa kilichotokea Liverpool ndio kilichopo kichwani kwangu”>>>Messi hata hivyo fainali ya Champions League itakayozikutanisha timu za Liverpool na Tottenham June 1 2o19 katika jiji la Madrid Hispania wacheaji wake wote wana goli chache na hakuna uwezekano wa kufunga nyingi na kumpiku Messi hivyo ni kama tayari mfungaji bora.

Post a Comment

0 Comments