Windows

JE, NI BARCELONA AU VALENCIA BINGWA WA COPA DEL REY LEO?


Kampuni ya Star Media (T) Ltd imetangaza kuonyesha mchezo wa fainali ya Kombe la mfalme wa Uhispania maarufu kama Copa del Rey. Mchezo huo utakaozihusisha timu za Barcelona na Valencia utapigwa Jumamosi hii saa 4:00 Usiku.

Barcelona ambao wamenyakua kombe la La Liga kwa msimu huu bado wana kazi ya kuwaridhisha mashabiki wao ambao bado wana majonzi ya kutolewa kwenye ligi ya mabingwa baada ya kuongoza kwa goli 3 katika mchezo wa kwanza na kuruhusu goli 4 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool.


Mbali na morali kuwa chini Barcelona wana orodha ndefu sana ya majeruhi ambao miongoni mwao ni wachezaji wa kikosi cha kwanza, mshambuliaji Luis Suarez, golikipa Ter Stegen (maumivu ya goti), Ousmane Dembele (maumivu ya misuli ya nyuma ya goti ‘hamsring’) na kiungo wa kati Arthur (maumivu ya nyonga).


Hata hivyo Barcelona bado wana kikosi kizuri sana licha ya majeruhi walionao. Nahodha Lionel Messi amekuwa kwenye kiwango bora kabisa msimu huu baadaya kupachika mabao 36 katika ligi na kuisaidia timu yake kushinda taji hilo.

Kwa Valencia hii ni fainali yao ya 16 katika Kombe la Mfalme huku wakiwa wamefanikiwa kulichukua mara 7 na kupoteza fainali 9. Mara ya mwisho Valencia kuwafunga Barcelona katika fainali za Copa delo Rey ilikuwa mwaka 1958 ambapo walishinda 3-0.


Kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania mchezo huu utaoneshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes katika chaneli ya ST World Football LIVE kuanzia saa 4:00 Usiku siku ya Jumamosi tarehe 25 Mei.
Chaneli ya ST World Football inapatikana katika kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa Dish na kifurushi cha UHURU kwa wateja wa Antenna.

Post a Comment

0 Comments